Benson Kipruto Ashinda Mbio za Tokyo Marathon 2024 na Kuweka Rekodi Mpya
Na Vincent Getiro
Mkenya Benson Kipruto aliibuka mshindi wa mbio za wanaume Tokyo, Japan tarehe 3,03,2024.
Benson aliweka rekodi ya 2:02:16 katika mbio hizo zilizowashirikisha wakimbiaji zaidi ya alfu thelathini.
Wakenya wengine waling'aa na kupeperusha bendera ya kenya katika nafasi ya pili na nne. Timothy Kiplagat alimaliza nafasi ya pili kwa masaa 2:02:55 naye Vincent Kipkemoi akimaliza wa tatu kwa masaa 2:04:18.
Ethiopia iliwakilishwa nafasi ya nne na tano naye Hailemaryam Kiros naye Tsegaye Getachew ambao walimaliza kwa masaa 2:05:43 na 2:06:25.
Aidha, Bethwel Kibet alimaliza nafasi ya 6 kutoka, Haimro Alafe nafasi ya 7 kutoka Israel, Simon Kariuki nafasi ya 8 kutoka Kenya, Yusuke Nishiyama kutoka nafasi ya 9 Japan huku Eliud Eliud Kipchoge akimaliza wa 10 katika mbio hizo.
Kwa upande wa wanawake Sutime Kebede wa Ethiopia alimaliza wa kwanza kwa masali 2:15:14 akifuatiwa naye mkenya Rosemary Wanjiru akimaliza wa pili kwa masali 2:16:14.
Amane Beriso wa Ethiopia alimaliza wa tatu kwa masali 2:16:58.
Ethiopia walikuwa na wakimbiaji wanne ambao walimaliza katika nafasi ya kumi bora. Maseret Abebayahau alimaliza wa 7 naye Tigist Abaychew alimaliza wa 9.
Aidha, Sifan Hassan wa Nertheland alimaliza wa nne, Besty Saina wa USA alimaliza wa 5, Hitomi Niiya wa Japana alimaliza wa 6, K. Galbadrakh akimaliza wa 8 naye Ayumi Morita akimaliza wa kumi kutoka Japan.