Chelsea Yalenga Nusu Fainali ya Kombe la FA Baada ya Kuwapepeta Leeds 3-2

Chelsea Yalenga Nusu Fainali ya Kombe la FA Baada ya Kuwapepeta Leeds 3-2
Wachezaji wa timu ya Chelsea wakisherehekea bao lao la tatu dhidi ya Leeds United katika uwanja wa Stamford Bridge usiku wa jana   katika mechi iliyokamilika kwa ushindi wa 3-2  Jumatano 28,2024

Na Mwana wa Africa 

Chelsea 3-2 Leeds: Chelsea ilitoka nyuma na kuwapepeta Leeds United katika mechi ya kombe la FA iliyosakatwa katika uwanja wa Stamford Bridge usiku wa jana tarehe Februari 28, 2024.

Baada ya Chelsea kukubali kichapo cha 1-0 jumapili 25 na Liverpool katika fainali ya Kombe La Carabao, walirejea  kwa vishindo  ugani Stamford Bridge na kuipepeta Leed United 3-2 usiku wa jana Alhamisi 29 2024. 

Chelsea ambao wameshikilia nafasi ya kumi na moja kwa alama  walitoka nyuma na kuwapepeta Leeds United ambao walishuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Uingereza msimu uliopita. Vijana hao wa Pochettino watacheza robo fainali na Leicester City ambao waliwabandua limbukeni Bournemouth ugenini kwa bao 1-0. 

Aidha, Manchester United waliipepeta Nottingham Forest 1-0 na kutinga robo fainali usiku wa jana. Bao la United lilifungwa na Casemiro dakika ya 89. Manchester United watapambana na Liverpool tarehe 16 Machi ugani Old Trafford.  Mabingwa hao wa Carabao mara kumi, waliipepeta Southampton ugani Anfield 3-0 na kutinga robo fainali. 

Liverpool ambao wanalenga kunyakua kombe la Uingereza, pia wanalenga kunyakua Kombe La FA kufikia mwisho wa msimu huu ambapo kocha Jurgen Klop ataondoka baada ya miaka 25. Liverpool wanaongoza ligi kuu kwa alama 60 alama moja mbele ya mabingwa watetezi Manchester City. 

Manchester City pia walitinga robo fainali jumanne 25 baada ya kuwapepeta Luton Town magoli 6-2 egenini huku Erling Haaland akifunga matano na kujiweka katika orodha wa wafungaji bora wa kombe hilo. 

Vijana wa Pep, watacheza na Newcastle United tarehe  16 Machi saa kumi na mbili. Newcastle ambao waliwabandua vigogo hao katika kombe la Carabao kwa bao 1-0 mwaka uliopita,  walijinyakulia tiketi ya robo fainali kupitia matuta ya penalti dhidi ya Blackburn. 

Aidha, Wolverhampton waliwabandua Brighton dakika ya 2 kupitia mchezaji Lemina na kutinga robo fainali usiku wa jana. Wolves watacheza na Coventry tarehe 16 Machi.