City Yaipa Arsenali Kiwewe

City Yaipa Arsenali Kiwewe
Wachezaji wa timu ya Manchester City

Na Mwana Wa Africa

Manchester City imepiga hatua kubwa ya kunyakua taji la Ligi Kuu Uingereza msimu huu kwa mara nyingine baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Tottenham    usiku wa jana. 

Mchezaji Erling Haaland ambaye anawania tuzo ya mfungaji bora alifunga  magoli  mawili, moja likiwa ni kwa njia ya penalti baada ya Jeremy Doku kuchezewa visivyo katika eneo la hatari. Kwa sasa, Staa huyo ana magoli 27. 

Kwa sasa, Arsenal na City ziko kwenye ushindani mkali msimu huu wa kunyakua taji huku ikiwa imesalia mechi moja pekee kwa kila mmoja ili Ligi Kuu ya Uingereza kukamilika.  

Ligi hiyo itakamilika jumapili na mshindi kati ya Manchester City na Arsenal atanyakua taji la EPL. 

Mabingwa hao watetezi wanalenga kuvunja historia nyingine ya kunyakua taji mara nne mfululizo siku ya Jumapili ambapo watakuwa na kubarua nyumbani dhidi ya West Ham katika uwanja wa Etihad nayo Arsenal kupapurana ugani  Fly Emirates dhidi ya Everton ambayo ilinusurika rasmi kushushwa daraja baada ya kuwapepeta Liverpool 2-0.

Baada ya Tottenham kupoteza, Aston Villa imefuzu kucheza katika kombe la Klabu Bingwa Ulaya  tangu mwaka 1999.  Kocha   Unai Emery amepigiwa upato sana katika klabu hicho tangu  alipoanza kukinoa kikosi cha Aston Villa. Tottenham watacheza UEFA Europa League msimu ujao. 

Kutokana na matokeo hayo, Vijana wa  Pep wanaongoza kwenye jedwali kwa alama 88, alama mbili mbele ya Arsenal ambayo inawafuata kwa ukaribu na alama 86.