Jaramogi Yaipapura Kisii Fainali ya KUSA Western Conference

Jaramogi Yaipapura Kisii Fainali ya KUSA Western Conference
Timu ya chuo kikuu cha Jaramogi na ile ya chuo kikuu cha Kisii. Picha Mwana wa Africa

Na Mwana wa Afrika

Chuo cha Jaramogi (JOOUST) kilifuzu kushiriki mashindano ya mpira wa mikono yatakayoandaliwa Masinde Muliro tarehe 29 Machi mwaka huu, baada ya kuwashinda wapinzani wao wa jadi, Chuo Cha Kisii, kwa alama 25-23 katika uwanja wa mpira wa mikono wa Kisii.

JOOUST walionekana kuwa na nguvu zaidi kuliko vijana wa Kisii katika kipindi cha mchezo kutokana na msukumo wa mashabiki wao ambao walifurahia ushindi baada ya mchezo kukamilika.

Jaramogi waliibuka kama nafasi ya pili katika kundi A, ambalo awali Kisii ilikuwa inaongoza, kabla ya kufuzu nusu fainali na hatimaye fainali.

Timu hizo mbili zilikutana tena katika fainali baada ya Jaramogi kuwashinda Maseno kwenye nusu fainali kwa alama 34-33. Kisii pia walishinda Kaimosi Friends katika nusu fainali kwa alama 27-18.

Aidha, Maseno walicheza na Kaimosi Friends katika mechi ya kusaka nafasi ya tatu kwenye mashindano hayo, ambapo Maseno walitwaa nafasi hiyo kwa kuwashinda Kaimosi 24-22.

Kulingana na ratiba ya mashindano ya KUSA Western Conference, timu zilizomaliza nafasi ya kwanza na ya pili ndizo zitakazowakilisha shule zao katika mashindano ya kitaifa yatakayoandaliwa na Masinde Muliro. Hata ingawa Kisii hawakushinda fainali, wamefuzu kwa kumaliza nafasi ya pili.