Manchester United Yatamba Dhidi ya Wolverhampton na Kufunga Bao la Ushindi Dakika za Mwisho
Na: Mwana Wa Afrika
Manchester United waliwadhibu vibaya Wolverhampton nyumbani, huku K. Mainoo akifungia Manchester United bao la ushindi katika mechi ya usiku wa jana. Mechi ilimalizika 3-4 katika uwanja wa nyumbani wa Wolverhampton, Molineux.
Wolverhampton hawajawahi kupoteza mechi nyumbani tangu walipopoteza 3-1 dhidi ya Liverpool Septemba 16. Manchester United walivunja rekodi hiyo dakika ya 96 kupitia kwa mchezaji Mainoo, aliyefunga bao lake la kwanza na la ushindi kwa mashetani wekundu.
Rashford aliwaweka United kifua mbele dakika ya 5, naye Højlund akiongeza la pili dakika ya 22. Manchester United walimaliza safari yao baada ya Casemiro na Højlund kufunga, lakini mabao yote mawili yalikataliwa.
Licha ya Sarabia kuwapa Wolverhampton matumaini ya kurejea mchezoni dakika ya 71 kupitia kwa mkwaju wa penalti, McTominay aliingia dakika 3 baadae kutoka kwenye benchi na kuwaweka Manchester United huru kwa 3-1 dakika ya 75 baada ya kupiga kichwa mpira wa kona uliochongwa na B. Fernandez.
Wolverhampton walijibu yote haya chini ya dakika 15, baada ya Kilman kusababisha 3-2 dakika ya 85, na Neto kuleta furaha ugani Molineux kwa kuwarejesha mchezoni Wolverhampton dakika za mazidadi kabla ya kipenga cha mwisho baada ya Casemiro kufanya kosa na kusababisha penalti. Dakika ya 96, mechi ilikuwa 3-3.
Mainoo alirejesha furaha ya mashetani wekundu na mashabiki dakika ya 96 baada ya kufunga goli la ushindi (3-4). Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18, amekuwa nguzo muhimu tangu Casemiro alipopata jeraha na kulazimika kukaa nje kwa muda. Ten Hag amekuwa akimtumia Mainoo kutokana na ubora wake.
Kutokana na ushindi huo, Manchester United wamepanda hadi nafasi ya 7 kwa alama 35, alama moja nyuma ya West Ham ambao walitoka sare ya 1-1 usiku wa jana dhidi ya Bournemouth.