Raga Kuanza Mara tu Shule Zitakapofunguliwa

Raga Kuanza Mara tu Shule Zitakapofunguliwa

Na Vincent Getiro

Kamati ya michezo ya kaunti ya Vihiga imetangaza kuwa michezo ya Raga kwa timu za shule za sekondari yenye wachezaji 15 kila upande itaanza tarehe 6 Machi 2024, baada ya likizo fupi na kufunguliwa kwa shule.

Michezo hiyo itaandaliwa katika shule ya wavulana ya Vihiga, ambayo ni mabingwa watetezi wa kombe hilo la wachezaji kumi na tano kila upande. Wanalenga kuhifadhi taji lao katika Kundi B.

Bodi ya Michezo ya Vihiga tayari imefanya na kugawa shule husika katika makundi mawili. 

Shule za Ebuboyi, Senende, Vijana wa Chavakali, Kegoye na Esalwa zimejumuishwa katika Kundi A, huku mabingwa watetezi Vihiga wamejumuishwa na shule za Ebusiloli, Mbale Highschool, Hobunaka na Nga'ng'ori katika Kundi B.