Rasmus Højlund Azidi Kutamba

Rasmus Højlund Azidi Kutamba
Mchezaji Rasmus Højlund na Alexander Garnacho wakisherehekea bao la pili na la ushindi dhidi ya Luton mechi ambayo ilitamatika 1-2 Jumapili 18, Februari 2024

Na Mwana Wa Afrika 

Rasmus Højlund, 21  anaendelea kuleta furaha Old Trafford  kwani mashabiki wa Manchester United  wemekuwa wakipendezwa na matokeo yake katika mechi za hivi karibuni. Hii ni baada ya Højlund kuwa mchezaji wa kwanza mchanga kufunga mara sita mfululizo katika mechi ambazo wamecheza ugenini na nyumbani.

Højlund alianza kutamba Januari 28, 2024  katika kombe la FA alipofunga dakika 93' dhidi ya Newport na mechi ikatamatika 2-4. Katika mechi za uingereza ambazo amefunga ni ikiwemo mechi dhidi ya Wolverhampton dakika ya 22; West Ham dakika ya 23;  Aston Villa dakika ya 17 na  mawili jumapili 18, 2024 dhidi ya Luton mabao ambayo yaliwafaidi mashetani wekundu kusajili ushindi kwa mara ya tano. 

Rasmus Højlund mwenye umri wa miaka 21 alizungumza na Sky Sport  na kusema," ushindi huu utatusaidia kuziba mwanya wa alama kati yetu na Tottenham..."

Tottenham walipoteza 1-2  nyumbani  dhidi ya Wolverhampton jumamosi 17, 2024. Tottenham wako nafasi ya tano kwa alama 47 alama tatu mbele ya  Manchester United ambao wamepanda hadi nafasi ya sita kwa alama 44. 

"Tutaendelea kuleta msukumo huo huo hadi tuvuke hatua nne bora. Hii itatusaidia kushiriki kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya. Ushirikiano mzuri umekuwepo kati ya Garnacho, Rashford, Bruno Fernandes, na mimi..." aliongeza Højlund akizungumza na Sky Sport.

Manchester United wanatazamia ushindi tarehe   28, Februari, 2024 ambapo watawakaribisha Fulham katika uwanja wa Old Trafford saa kumi na mbili jioni.